Monday, July 1, 2013

HALMASHURI YA WANGING'OMBE YAANZA RASMI.

Halmashuri ya Wanging'ombe imeanza rasmi leo,baraza la Madiwani lilio kaa juzi katika Ukumbi wa Njombe Halmashauri liliweza kuwagaa Madiwa wa kuanzisha Halmashuri hiyo mpya.

Katika kikao hicho cha baraza waliweza kuchaguliwa Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wanging'ombe na Makume wake pamoja na kamati mbalimbali ziliunda.

Picha  za kikao cha Madiwani chini.








Saturday, June 29, 2013

AFYA YA NELSON MANDELA BADO TETE...!!

AFYA YA NELSON MANDELA BADO TETE...!!


Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita.
Baada ya kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia jamaa zake wanapomuita huku akijaribu kufungua macho yake.
Makaziwe amesema “Nimekasirishwa sana. Kwa sababu Mandela ni kiongozi mashuhuri duniani, haimaanishi utu wake udhalilishwe pamoja na kuvuka mipaka kuingilia mambo yake binafsi. Hapa naona kuna ubaguzi wa rangi, huku vyombo vingi vya kimataifa vikivuka mipaka, ni kama ndege aina ya Tai au Vulture wanaosubiri Simba kumla mnyama aliomuwinda kisha wakimbilie mzoga.
Wamevuka mipaka ya maadili. Wakati hayati Margaret Thatcher alipokuwa mgonjwa mbona sikuona, ukaribu wa vyombo vya habari kiasi ninachokiona kwa banangu? Ni kwa sababu hii ni nchi ya kiafrika. Wanahisi kuwa hapa wanaweza kuvuka mipaka wanavyotaka, '' alisema Makaziwe
Mapema jana, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma alifutilia mbali ziara yake ya kwenda Msumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbaya kiafya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj alisema kuwa hali yake imedorora zaidi.

Mandela ambaye ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela.
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"Tutasikitika sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijana John Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua kuahirisha safari yake.
Taarifa kutoka kwa ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika Kusini wanaoendelea kuiombea familia ya Madiba.

Uamuzi wa Rais Zuma kufutilia mbali ziara yake ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa kikanda kuhusu uwekezaji anaonyesha wazi kuwa hali ya Mandela inaendelea kuzorota.

MKASA WA BINTI ALIYENUSURIKA KUNYONGWA NA MUMEWE AMBAAYE AMBAYE NI ASKARI MPELELEZI HUKO IRINGA...!!

Thursday, June 27, 2013 | 2:38 AM

Hapa Rehema akiwa wodini katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alipokimbizwa kwa matibabu kutokana na kipigo kikali toka kwa askari huyo Hapa akionekana mwenye uvimbe zaidi Hapa akionyesha majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo Hapa akiwa hoi kwa kipigo



Bi Rehema Shauri Madongo mkazi wa Wilolesi mjini Iringa akiwa na mtoto wake baada ya kuponea katika tundu la sindano kuuwawa kwa kipigo kutoka kwa mmewe ambaye ni askari polisi mjini Iringa kiasi cha kukimbia nyumba na kurudi kwa wazazi wake

stepen kanyala akiwa na mke wake siku ya harusi yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa

Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha

Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri


Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .

" Mimi niliolewa kwa ndoa na Stephen Kanyala ambae ni askari kitengo cha upelelezi ila baada ya kuolewa ukiwa umepita mwezi mmoja tuo nilianza kushuhudia mateso ya ndoa kutokana na kipigo na mateso makali niliyokuwa nikiyapata"

Anasema kuwa kila wakati pindi anapotaka kujua jambo kutokana kwa mume wake huyo hasa pale anapoona jumbe zenye utata katika simu yake ambazo zimetoka kwa wanawake anaiowatambua vizuri amekuwa akijibiwa kwa kipigo kikali. Rehema alisema kuwa ni rahisi kwake kuweza kuhesabia siku ambazo hajapigwa kuliko kuhesabi siku ambazo amepigwa ambazo ni nyigi zaidi .

Kwa alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba.

" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"

Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama. Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua .

Alisema kuwa baada ya kujifungua mtoto wa njia ya Oparesheni mwanaume huyo alimpiga kiasi cha kumjeruhi mtoto wa mwezi mmoja kwa kumpiga kofi ambalo lilielekezwa kwake na bahati mbaya likaishia kwa mtoto. Aidha alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na polisi kulindana na kuwa suala hilo la askari polisi kulindani lilianza toka wakati kamanda wa polisi akiwa Evarist Mangala ,pia alipofika kamanda Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa amehamishwa baada ya cheo kupanda pia amepata kufikisha malalamiko yake ila hakuna jipya ila sasa amefikisha tena suala hilo kwa kamanda mpya RPC Ramadhan Mungi ambae amedai kuwa na imani nae zaidi katika kulishughulikia suala lake Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake .

Hivyo alisema katika kunusuru uhai wake kwa sasa ameamua kurudi kwa wazazi wake na suala la ndoa hataki tena .
Kwa upande wake Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri alisema kuwa amechoka kuuguza binti yake kwa kipigo na kuwa kuna wakati mwanaume huyo amekuwa akitishia kumpiga hata yeye.

Hivyo alisema kwa sasa mbali ya kumtoa binti yake Hospital ila wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara kuwa dawa yao inachemka na ipo siku wataonja mauti.

Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo . Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa ila askari wenzake wanamlinda.

Kuhusu uamuzi wa binti yake wa kuomba ndoa hiyo kuvunjwa alisema anaungana na binti yake kuikataa ndoa hiyo na kuwa kwa sasa wapo tayari kurudisha mahali yake ya Tsh 200,000 ambazo alizitoa kama mahali ili kunusuru uhai wao na uhai wa mtoto wake huyo.

Friday, June 28, 2013

MWILI WA MAREHEMU MEXON NYEKELELA CHOTA ULIOZAMA KWENYE MAJI KATIKA BWAWA LA KAMPUNI TANWAT UMEPATIKANA

MWILI WA MAREHEMU MEXON NYEKELELA CHOTA ULIOZAMA KWENYE MAJI KATIKA BWAWA LA KAMPUNI TANWAT UMEPATIKANA BAADA YA SIKU TANO KUPITA TANGU UZAME NA MAZISHI KUFANYIKA JANA HIYOHIYO KATIKA MTAA WA KIBENA MJINI NJOMBE.











picha ya zamani ya marehemu Chota.

MAREHEMU Mexon Chota katika picha yake aliyopiga siku za karibuni kabla hajazama kwenye bwawa la kampuni ya Tanwat akiwa na mama yake.




JITIHADA ZA WANANCHI WAKATI ZILIPOKUWA ZINAFANYIKA ZA KUUTAFUTA MWILI WA MAREHEMU MEXON CHOTA.





HATIMAE MWILI WA MAREHEMU WAPATIKANA SASA WANAUTOA MBELE YA BOAT NI MTAALAM TOKA WILAYANI MUFINDI AKIWA AMESHIKIRIA NGUO YA MAREHEMU  TAYARI KWA KUTOKA NAO NJE YA MAJI.













TAYARI WAMEFANIKIWA KUUTOA KWENYE MAJI NA HAPA WANAULAZA KWENYE KARATASI ILI MAJI YAPUNGUE MWILINI MWAKE MAREHEMU MEXON CHOTA.



TAYARI WAMEKWISHA UFUNIKA MWILI WA MAREHEMU USIWAKIWE NA JUA NA KUGUSWA NA WADUDU KAMA NZI KWA KUWA ULIANZA KUHARIBIKA.



AFISA UPELELEZI  WA JESHI LA POLISI WILAYA YA NJOMBE PHELISIAN KAMGISHA  AKIWA AMEONGOZANA NA DR WA KIBENA WAKIWASILI ENEO LA TUKIO KUUPIMA MWILI WA MAREHEMU NA KUUOSHA TAYARI KWA MAZISHI.

AFISA TARAAFA WA NJOMBE MJINI LILIANI NYEMELE KWA MASIKITIKO MAKUBWA ANASOGEA KWENYEN MWILI WA MAREHEMU .



MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEKWISHA OSHWA NA TAYARI KWA KUAGWA.





WANANCHI NA NDUGU WANAUAGA MWILI WA MAREHEMU KATIKA BWAWA HILO ALIKOOKOLEWA.


AFISA TARAAFA WA NJOMBE MJINI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI BAADA YA MWILI KUANDALIWA KWENDA KWENYE  MAZISHI.





HAWA WATATU NI WATAALAM WA KUZAMA NDANI YA MAJI TOKA DAR MWENYE SUTI NYEUSI NI JOSEPH MAPUNDA ALIEONGOZA MSAFARA HUO NA WAWILI WATUMISHI WENZAKE.


KOTI NA VIATU KWAAJILI YA KUZUIYA BARIDI UKIWA NDANI YA MAJI NA VIATU KUZUIYA MIGUU ISIHARIBIKE UKIWA NDANI YA MAJI AMBAPO MTUNGI HUU UNA KILOGRAM 15 UNABEBWA NA KUZAMA NAO NDANI YA MAJI UKIWA UMEJAZWA HEWA SAFI YA KUVUTA MWANADAMU SAWA NA AKIWA NJE YA MAJI.


MTUNGI WA GESI KWAAJILI YA PUMZI WAKATI AKIZAMA NDANI YA MAJI NA UTUMIAPO HEWA YA MTUNGI HUU UNAUWEZO WA KUKAA ZAIDI YA SAA MOJA UKIWA KWENYE MAJI



BAADA YA KUWASILI WATAALAM TOKA DAR ES SALAAM  DIVE INSTRUCTOR SEA BREASE MARINE JOSEPH MAPUNDA NA WENZAKE WAWILI WAKAANZA KUTOA ELIMU KWA UCHACHE BAADA YA WANANCHI KUTAKA KUFAHAMU MATUMIZI YA VIFAA WALIVYOKUJA NAVYO KUOKOLEA MWILI WA MAREHEMU.








MCHUNGAJI WA KANISA LA KILUTHEL TANZANIA USHARIKA WA KIBENA K.K.K.T NELSON KADUMA ALIONGOZA IBADA YA MAZISHI NA HAPA ANAWEKA MSALABA KWENYE KABURI LA MAREHEMU.




MAMA YAKE MAREHEMU MEXON CHOTA BI.LAINES MLIMBILA AKIWEKA TAJI KWENYE KABURI LA MTOTO WAKE ALIYEKUFA MAJI.Picha na Michael Ngilangwa.




Mazishi ya Mkazi Mmoja wa Kibena Mjini Njombe Mexon Nyekelela Chota Yamefanyika Leo Katika Makaburi ya Kibena,Ikiwa ni Baada ya Kupatikana Kwa Mwili wa Marehemu Uliokuwa Amezama Kwa Siku ya Tano Katika Mabwawa ya Kampuni ya TANWAT Mjini Njombe.

Mwili wa Marehemu Ulipatikana Leo Majira ya Saa Nane Mchana Ikiwa ni Baada ya Jitihada za Muda Mrefu za Wananchi na Viongozi Kuweza Kuutafuta Mwili Huo Bila Mafanikio Kutokana na Ukosefu wa Vifaa Vya Uokozi.

Akizungumza Mara Baada ya Kupatikana Kwa Mwili Huo Afisa Tarafa ya Njombe Mjini Bi Lilian Nyemele Ameishukuru Kampuni ya TANWAT Kwa Namna Ilivyoshiriki Katika Kusaidia Zoezi Hilo Pamoja na Wananchi Wote Walioshiriki.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwasili Mkoani Njombe Mtaalam wa Uzamiaji Kutoka Jijini Dar Joseph Mapunda Anasema Kuna Haja Kwa Serikali ya Mkoa wa Njombe Kuanza Kutoa Mafunzo Kwa Wananchi na Wataalam Mbalimbali Ili Kuweza Kupata Wataalam wa Uzamiaji.

Aidha bwana Mapunda amesema fursa za kupata mafunzo ya kuogelea na uzamiaji ndani ya maji zinapatikana Dar es salaam ambapo taasisi na serikali zinatakiwa kuwaita wataalamu hao kufika mahala walipo wananchi na vijana na kupatiwa mafunzo hayo ili kuwapata vijana wenye utaaramu huo ikiwemo wananchi wenyewe kuwapeleka vijana wao kwenye vyuo hivyo ili kupata mafunzo hayo.

Kwa upande wao viongozi wa mitaa ya Kibena Pasval Kaduma na Faustini Mwenda wamesema kufuatia kutokea kwa tukio hilo la kuzama kwa kijana hiyo kampuni ya Tanwat kwa kushirikiana na viongozi wa serikali wasema haruhusiwi mtu yeyote kwenda kuvua samaki wala kuogelea katika mabwawa hayo kinyume na hapo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Marehemu Mexon Nyekelela Chota Alizama Kwenye Mabwawa Hayo Mnamo March Mosi Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi na Moja Jioni Wakati Akiwa na Wenzake Mara Baada ya Kumaliza Shughuli Zao za Sanaa na amepatikana jumanne march 5 na kuzikwa katika makaburi ya eneo la   kanisa la romani  la zamani mtaa wa kibena kati mjini Njombe.