Thursday, October 19, 2023

CNG IPEWE KIPAUMBELE KUENDESHA MITAMBO NA MAGARI NCHINI- KAMATI YA BUNGE

CNG IPEWE KIPAUMBELE KUENDESHA MITAMBO NA  MAGARI NCHINI- KAMATI YA BUNGE


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeishauri Serikali kuweka kipaumbele katika kusambaza Vituo vya Nishati ya Gesi Iliyoshindiliwa (CNG) inayotumika katika kuendesha mitambo na magari nchini ili kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mafuta pale zinapotokea.

Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 18, 2023  jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mathayo David wakati Kamati hiyo ilipopokea taarifa ya Wizara ya Nishati, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa kuanzisha vituo hivyo. 





“Tunashauri Serikali iweke kipaumbele katika matumizi ya gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na matumizi mengine ili Watanzania waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi,” amesema Mwenyekiti wa Kamati,  Mathayo David.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mathayo ameipongeza Serikali kwa mikakati mizuri ya uanzishwaji wa karakana za kubadili mifumo ya matumizi kutoka kwenye mafuta na kwenda kwenye gesi asilia kwenye magari hali  inayochochea matumizi ya gesi asilia nchini kwa wingi. 

"Uwepo wa karakana hizi kwa wingi utarahisisha utoaji wa huduma za ubadilishaji mifumo na ukarabati wa hitilafu kwa muda mfupi na karakana hizi zitumie teknolojia ya kisasa wakati wa kubadili magari na mitambo,” ameeleza Mhe. Mathayo.


Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali imepokea ushauri wote uliotolewa na kamati ili kuweza kuboresha Sekta ya Nishati nchini.  

Amesema, Wizara imedhamiria kuchochea matumizi ya Gesi Asilia iliyoshindiliwa kwa maeneo pia  yaliyo mbali na mtandao wa mabomba pamoja na matumizi ya gesi hiyo kwenye magari kwa kuwa na vituo vingi vya kujazia gesi kwenye magari. 


Viongozi mbalimbali walioshiriki katika kikao hicho ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Bw. Athumani Mbuttuka, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga na Watendaji kutoka Wizara na Taasisi.

Monday, October 18, 2021

TPA WATAKIWA KUJIPANGA KUFANYA BIASHARA


TPA WATAKIWA KUJIPANGA KUFANYA BIASHARA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini kujipanga kufanya biashara ili kukidhi malengo ya Serikali ya kutumia lango la bandari kukuza uchumi wa nchi na wakazi wake.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga na kukarabati miundombinu ya bandari hivyo ni wakati sasa kwa watendaji na watumishi wa bandari kuleta biashara kubwa nchini itakayoleta faida na kuhuisha uchumi wa sekta nyingine.

“Ni wakati wa idara ya masoko ya bandari na watumishi wake kufanya kazi kimkakati wakilenga kufanya biashara na kuzalisha faida”, amesema Prof. Mbarawa.

Amezungumzia umuhimu wa watendaji wa bandari kuweka wahitimu wa fani za uhandisi katika miradi ya ujenzi inayoendelea ili kuwajengea watanznia uwezo.

Zaidi ya shilingi bilioni 440 zitatumika katika ukarabati mkubwa wa bandari ya Tanga na kukamilika huko kutawezesha meli nyingi na kubwa kutumia bandari hiyo na kufufua uchumi wa mkoa huo.

Amezungumzia umuhimu wa uadilifu, ubunifu na uzalendo kwa watumishi wa bandari ili waweze kushindana na bandari nyingine na kupata tija.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima amemhakikishia Waziri wa Ujenzi  na Uchukuzi kuwa mkoa huo utahakikisha unaweka mazingira salama na rafiki kwa wakandarasi wanaojenga miundombinu mkoani humo ili kufikia malengo ya kimkakati ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Prof. Mbarawa alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Tanga kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, vivuko, uwanja wa ndege na bandari. 


 

Monday, July 1, 2013

HALMASHURI YA WANGING'OMBE YAANZA RASMI.

Halmashuri ya Wanging'ombe imeanza rasmi leo,baraza la Madiwani lilio kaa juzi katika Ukumbi wa Njombe Halmashauri liliweza kuwagaa Madiwa wa kuanzisha Halmashuri hiyo mpya.

Katika kikao hicho cha baraza waliweza kuchaguliwa Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wanging'ombe na Makume wake pamoja na kamati mbalimbali ziliunda.

Picha  za kikao cha Madiwani chini.