Friday, June 28, 2013

JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LINAMSHIKILIA MAMA MMOJA KWA TUHUMA ZA KUMTUPA MTOTO MCHANGA

JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LINAMSHIKILIA MAMA MMOJA KWA TUHUMA ZA KUMTUPA MTOTO MCHANGA BAADA YA KUJIFUNGUA HUKU MMOJA AKISHIKILIWA KWA UBAKAJI.,WAWILI WAFARIKI KWA AJALI






 







 MASHUHUDA WA TUKIO WAKIWA PAMOJA NA ASKALI WA POLISI MKOA WA NJOMBE
MWENYEKITI WA MTAA WA NATIONALHOUSING MJINI NJOMBE BWANA MAKWETA AKIZUNGUMZA BAADA YA KUOKOTWA MWILI WA MTOTO MCHANGA HUYO.

Watu Watatu Wamefariki Katika Matukio Matatu Tofauti Mkoani Njombe Likiwemo la Mtoto Mchanga Aliyeokotwa Akiwa amekufa Eneo la  Nationalhousing Mjini Njombe Huku Wengine Tisa Wakiwa wamejeruhiwa na Kulazwa Katika Hospitali Mbalimbali za Mkoa wa Njombe Baada ya Gari Walilokuwa Wakisafiria Kupata Ajali.

Kaima Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Focus Malengo Amesema Katika Tukio la Kwanza Juni 22 Mwaka Huu Ambapo Mwanamke Mmoja Alijifungua Mtoto wa Kike na Kumtupa Nje ya Nyumba Anayoishi na Kwamba Jeshi Hilo Linamshikilia Kwa Mahojiano.

Kamanda Malengo Amesema Watu Wawili Wamefarika Kutokana na  Ajili za Barabara Ikiwemo Ajali ya Gari Lenye Namba za Usajili T 965 BDM Aina ya Noah Walilokuwa Wakisafiria Kuacha Njia na Kupinduka na Kusababisha Kifo cha Ambwene Mgaya na Kusababisha Majeruhi Tisa.

Amesema Ajali Hiyo Imetokea Juni 22 Majira Saa Moja na Nusu Usiku Katika Kijiji cha Iboma Barabara Kuu ya Njombe na Kwamba Gari Hilo Lilikuwa Likiendeshwa na Nesfoli Kayombo.

Aidha Kamanda Malengo Amesema Ajali Nyingine Imetokea Juni 22  Saa Moja Usiku Eneo la Shule ya Viziwi Mjini Njombe Ambapo Adam Mng'ong'o Akiwa Anaendesha Pikipiki Yenye Namba za Usajili T 532 BYT Amefariki Papo Hapo Baada ya Kugongwa na Gari 

Kaimu Kamanda Huyo wa Polisi Amesema Jeshi la Polisi Bado Linaendelea na Uchunguzi wa Matukio Hayo Huku Akiwataka Madereva Kufuata Sheria za Barabara na Kujali Watu Wengine Wanaotumia Barabara Hizo.

Wakati Huo Huo Jeshi Hilo Linamshikilia Mkazi wa Kijiji cha Mtila Sikujuwa Msemwa Kwa Tuhuma za Kumbaka Mtoto Wakike Mwenye Umri wa Miaka Mitatu na Kumsababishia Maumivu Makali.

Kaimu Kamanda Malengo Amesema Tukio Hilo Limetokea Juni 22 Majira ya Saa Sita Mchana Kijijini Humo na Kwamba Mtoto Huyo Amelazwa Kwa Ajili ya Matibabu.

JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LIMEAHIDI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WANAWEKA VITUO VYA MABASI ENEO LA MTO RUHUJI NA VITUO VISIVYO RASMI


JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LIMEAHIDI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WANAWEKA VITUO VYA MABASI ENEO LA MTO RUHUJI NA VITUO VISIVYO RASMI
















Licha ya jeshi la polisi kupiga marufuku kwa magari kuweka kituo eneo la Ruhuji lakini bado kuna baadhi ya madereva wa magari mbalimbali ya abiria na mizigo wanaendelea kupaki na kusubiria abiria eneo hili.

Na biashara ndogondogo zinaendelea eneo hili nihatari kwa usalama wa wafanyabiashara hao endapo magari yataendelea kuweka kituo kama cha kuchukulia abiria

HABARI ITAKUJIA HIVI PUNDE................

MIKAKATI NA MBINU MBALIMBALI DHIDI YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YAENDELEA KUJADILIWA MKOANI NJOMBE




Ajali mbaya yatokea katika eneo la maji masafi Kawetere Nje kidogo ya Jiji la Mbeya barabara ya Mbeya- Tabora Kichanga afariki dunia wengine wajeruhiwa.

CHANZO CHA HABARI HII NI MBEYA YETU BLOG


Mtambo wa Wachina ukinyenyua gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.






Baadhi  ya abiria walionusurika  wakihamisha mizigo yao kutoka katika gari lililopata ajali ya Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.

Wachina wanaojenga barabara ya Chunya wakishangaa gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Majeruhi wa ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani.

Kondakta wa gari la Kampuni ya Sabena Seif Salum (34) akisaidia kuokoa mizigo ya abiria baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.

Gari la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
                             ********************************************
KICHANGA cha Miezi 6 kimefariki dinia papo hapo na wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa  katika ajali mbaya iliyohusisha Basi kampuni ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro  pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
 
Kwa mujibu wa Wahanga wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema imetokana na mwendokasi ambapo Dereva alishindwa kulimudu basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza.
 
Wamesema ajali hiyo imetokea majira ya Saa moja asubuhi  ambapo katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya huku wengine wakipatiwa huduma ya kwanza kisha kuendelea na safari baada ya kubadilishiwa gari.
 
Gari hilo lenye namba za usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa kuendelea na safari ndipo lilipoletwa basi lingine kampuni hiyo hiyo ya Sabena kwa ajili ya kuendelea na Safari.
 
Kondakta wa Basi hilo Seif Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari uliosababisha kupasuka kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa kusimama na kutumbukia mtaroni.
 
Amemtaja Dereva wa basi hilo kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa alikimbia baada ya ajali hiyo ingawa kondakta alitoa taarifa kuwa kafuata matibabu Hospitalini

Wednesday, June 26, 2013

MKURUGENZI WA HALMASHURI YA KILOLO AFARIKI

MKURUGENZI WA HALMASHURI YA KILOLO AFARIKI
Marehemu Mohamed Ngwalima aliyeshika kitabu enzi za uhai wake

Marehemu Mhamedi Ngwalima kutoka kulia akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya kilolo Mh.Gerad Guninita


kaimu mkurugenzi wa wilaya ya kilolo akiteta jambo na mwenyekiti wa halimashauri









 Watumishi  wa  Halmashauri ya  Kilolo na  wananchi mbali mbali  wakiwa  katika Hospital ya  mkoa  wa  Iringa  wakisubiri  kuaga mwili  wa mkurugenzi  wao

 Mwanasheria  wa mkoa  wa Iringa Bw Paul Lekamoi akiwa na  waombolezaji  wengine

 Mratibu  wa  Sensa mkoa  wa Iringa kulia akiwa na waombolezaji  wengine


 Mwenyekiti  wa Halmashauri ya  Kilolo Joseph Muhumba  kulia akiwa na kaimu mkurugenzi wa Kilolo

 Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akiwa katika msiba  huo hii kweli ni polisi jamii

   MAREHEMU MOHAMED SAID NGWALIMA
   Marehemu alizaliwa tarehe 16 februari 1957 ikwiriri rufiji na kupata elimu ya sekondari kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne katika shule ya sekondari same kuanzia mwaka 1978-1980 alipata elimu ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari shinyanga
   mwaka 1980 mpaka 1981 alitumikia taifa katika jeshi la kujenga taifa kabla ya kujiunga na masomo ya shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha dar es salaam,sgahada aliyotunukiwa mwaka 1986
  Mara baada ya kutunukiwa shahada ya uchum i mwaka 1986,aliajiriwa kama mchumi katika halimashauri ya wilaya ya Mtwara.
 Al;itumikia taifa katika maeneo mbalimbali kama mchumi mpaka mwaka 2007 alipoteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Mbulu.

  Mwaka 2012 alihamishiwa katika halimashauri ya wilaya ya Mtwara na mwaka huu 2013 alihamishiwa katika halimashauri ya wilaya ya kilolo ambako amekuwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo mpaka mauti ilipo mfika tarehe 25/06/2013 saa 1:15 jioni katika nyumba aliyokuwa anaishi na familia yake ilyopo karibu na ofisi za halimashauri hiyo
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA
Source FRANCIS GODWINI